Mark 1:21-26

21 aWakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya Sabato, mara Isa akaingia sinagogi, akaanza kufundisha. 22 bWatu wakashangaa sana kwa mafundisho yake, kwa maana aliwafundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wa sheria. 23 cWakati huo huo katika sinagogi lao palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, 24 dnaye akapiga kelele akisema, “Tuna nini nawe, Isa Al-Nasiri? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!”

25 eLakini Isa akamkemea, akamwambia, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” 26 fYule pepo mchafu akamtikisatikisa huyo mtu kwa nguvu, kisha akamtoka akipiga kelele kwa sauti kubwa.

Copyright information for SwhKC